info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

DKT. NDUMBARO APONGEZA TTCL KWA HUDUMA ZA MAWASILIANO KWA WAJUMBE WA IPU 2026

Na Debora Ngalima

Mwenyekiti wa Ujumbe wa Tanzania katika Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb),amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa namna linavyotoa huduma za mawasiliano kwa wajumbe na washiriki wa Mkutano wa IPU 2026 unaofanyika jijini Arusha.

Dkt. Ndumbaro alitoa pongezi hizo baada ya kutembelea banda la TTCL katika Mkutano wa IPU 2026, mapema leo Oktoba 8, 2026, ambapo alipata fursa ya kufahamu huduma  za mawasiliano zinazotolewa na Shirika hilo kwa ajili ya kuwezesha shughuli za mkutano.

Akiwa katika banda la TTCL Dkt. Ndumbaro alielezwa namna TTCL inavyoshiriki katika kuhakikisha wajumbe na washiriki wa mkutano wanapata huduma za mawasiliano zinazowawezesha kuwasiliana, kupata taarifa na kuendelea na shughuli zao za kidijitali kwa ufanisi wakati wa mkutano huo.

Dkt. Ndumbaro amepongeza TTCL kwa mchango wake katika kuwezesha mawasiliano wakati wa mkutano huo, akitambua umuhimu wa huduma za mawasiliano katika kufanikisha mikutano ya kimataifa yenye ushiriki wa viongozi na wabunge kutoka mataifa mbalimbali.

Ushiriki wa TTCL katika IPU 2026 unalipa Shirika nafasi ya kuonesha uwezo wake katika kutoa huduma za mawasiliano katika mazingira yenye mahitaji makubwa ya teknolojia, huku likiendelea  kuwahudumia washiriki wa mkutano huo muhimu.

Kwa TTCL, uwepo katika mkutano huo ni sehemu ya jitihada za kuonesha uwezo wa Shirika katika kutoa huduma za mawasiliano kwa taasisi, biashara na matukio makubwa nchini.

Mkutano wa IPU 2026 unaendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC), ukiwakutanisha viongozi na wabunge kutoka nchi mbalimbali kwa ajili ya kujadili masuala yenye umuhimu kwa mabunge na jamii kimataifa.