IPU 153 YAFUNGUA FURSA ZA KIMKAKATI KWA TTCL KUPITIA MKONGO WA TAIFA
Na Debora Ngalima
Leo, tarehe 7 Oktoba 2026, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Jimbo la Uyole na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) anayemaliza muda wake amekutana na Bi. Linda Mushi, akimwakilisha Meneja wa Mkoa wa TTCL Arusha, wakati wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Katika mazungumzo yao, walijadili pamoja na mambo mengine, umuhimu wa miundombinu imara ya mawasiliano katika kuchochea mageuzi ya kidijitali, kuwezesha huduma za kidijitali na kufungua fursa mpya za ushirikiano na biashara.
Kupitia ushiriki katika majukwaa ya kimataifa kama IPU 153, TTCL inaendelea kutumia fursa hizo kutangaza uwezo wa miundombinu na huduma zake, kujenga na kuimarisha mahusiano na wadau wa ndani na kimataifa, pamoja na kufungua fursa za biashara kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.