
KIMARA IMEITIKA: FAIBA MLANGONI KWAKO KUTOKA TTCL
Katika jitihada za kuleta mapinduzi ya kidigitali na kuboresha maisha ya Watanzania, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeanzisha Kampeni kabambe ya "Faiba Mlangoni Kwako" katika eneo la Kimara Stopover.
Kampeni hii inalenga kupeleka huduma ya intaneti ya kasi ya faiba moja kwa moja kwenye nyumba za wakazi wa Kimara – na kweli, Kimara imeitika!
Huduma hii ya kisasa ya TTCL inaleta suluhisho la mawasiliano bora, na unafuu wa gharama kwa jamii. Kwa sasa shirika linatekeleza ujenzi wa miundo mbinu ya mawasiliano ili kuwawezesha wakazi wa Kimara kupata fursa ya kufanikisha biashara zao kimtandao, kuwasiliana bila kikwazo, pamoja na kupata huduma mbalimbali kidigitali za kidigitali.
Faiba Mlangoni Kwako ni huduma inayozingatia familia, Wafanyabiashara na Wajasiriamali ambapo mpango huu mpango huu unapunguza gharama za mawasiliano kwa asilimia kubwa kutokana na TTCL kufunga kifaa (Router) maalum yenye uwezo wa kuunganisha hadi vifaa 32 kwa wakati mmoja jambo ambalo linaifanya familia nzima au Wafanyabiashara kufurahia mtandao wa kasi bila kikomo na kuondoka katika usumbufu wa kujiunga na mabando.
Kampeni hii haitaacha kundi lolote nyuma licha ya Wafanyabiashara na wajasiriamali, kwa upande wa Wanafunzi, Faiba Mlangoni Kwako ni daraja la kuelekea mafanikio ambapo wanaweza sasa kusoma mtandaoni, kushiriki madarasa ya kidigitali, kufanya utafiti, na kukuza maarifa yao wakiwa nyumbani kwao. Hii ni hatua muhimu ya kuziba pengo la elimu na kuongeza uelewa katika jamii.
Kipekee Kampeni ya Faiba Mlangoni Kwako katika maeneo ya Kimara si tu ni kampeni ya kupeleka mawasiliano eneo hilo, bali ni suluhishola kiteknolojia la maisha bora.