MHE. RAIS APITA BANDA LA TTCL, AWASALIMIA VIONGOZI NA WAFANYAKAZI
Na Adeline Berchimance
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasalimia Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) waliokuwa wakiliwakilisha Shirika katika banda la maonesho wakati wa Tamasha la Kizimkazi 2026.
Katika ziara yake kwenye mabanda mbalimbali ya maonesho, Mhe. Rais alipita katika banda la TTCL na kutoa salamu kwa timu iliyokuwepo. Ingawa ufinyu wa muda haukumruhusu kupata fursa ya kusikiliza kwa kina maelezo kuhusu huduma, bidhaa na ubunifu mbalimbali unaoendelea kutolewa na TTCL, uwepo wake na salamu hizo zilibeba heshima na kumbukumbu ya pekee kwa wafanyakazi wa Shirika.
Kwa TTCL, tukio hilo ni la kujivunia na linaendelea kuwa hamasa katika kutekeleza dhamira ya Shirika ya kuwaunganisha Watanzania kupitia huduma za kisasa, salama na zenye uhakika za mawasiliano, huku likichangia ukuaji wa uchumi wa kidijitali na maendeleo ya Taifa.