info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

NAIBU GAVANA WA BENKI KUU ATEMBELEA BANDA LA TTCL SABASABA 2026, APONGEZA MAGEUZI YA KIDIJITALI

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Rahma S. Mahfoudh, ametembelea banda la TTCL katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba 2026) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, na kujionea huduma mbalimbali za kidijitali zinazotolewa na Shirika.

Akiwa kwenye banda, Dkt. Mahfoudh amepongeza juhudi za TTCL katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini ambazo zimechangia kuharakisha mageuzi ya kidijitali na kuchochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini Tanzania.

TTCL tunamshukuru Naibu Gavana wa Benki Kuu kwa kutembelea banda letu na kwa kutambua mchango wa Shirika katika kujenga Tanzania ya kidijitali.

#Sabasaba2026
#ZaidiyaMaonesho
#Ishikidigitali
#MaoneshoYaBiashara
#mawasiliano