NAIBU WAZIRI MHE. WANU HAFIDH AMEIR ATEMBELEA BANDA LA TTCL KIZIMKAZI 2026
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Makunduchi, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, Zanzibar.
Katika ziara hiyo, Mhe. Wanu alipata fursa ya kujionea huduma na suluhisho mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na TTCL, pamoja na namna Shirika linavyoendelea kutumia teknolojia katika kurahisisha mawasiliano na kuwezesha shughuli za wananchi na taasisi.
Ziara hiyo imekuwa fursa muhimu kwa TTCL kueleza mchango wake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano na kuunga mkono maendeleo ya kidijitali nchini.
TTCL inatoa shukrani za dhati kwa Mhe. Wanu Hafidh Ameir kwa kutenga muda wake kutembelea banda la Shirika na kujionea huduma zinazotolewa kwa Watanzania.