RAIS SAMIA AZIAGIZA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA KUFANYA KAZI KWA UFANISI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 28,2024 amefungua rasmi Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma kilichofanyika jijini Arusha.
Kikao hiki kililenga kujadili na kuimarisha utendaji wa Mashirika ya Umma, kuweka mikakati ya kuboresha huduma kwa wananchi, na kuhakikisha taasisi hizo zinafanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kutekeleza mipango ya Serikali.
Akihutubia Taasisi na Mashirika ya Umma na Mashirika ya umma yapatayo 248, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa viongozi kuwa na uwajibikaji, ubunifu, na kujituma katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha alihimiza Bodi na Wakuu wa Taasisi kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili na kuhakikisha kwamba taasisi wanazoongoza zinatoa huduma bora na zenye tija kwa wananchi.
Kikao hiki ni sehemu ya juhudi za Rais Samia katika kuimarisha utawala na utendaji wa taasisi za umma ili ziweze kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya Taifa.