info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TANZANIA YAFUATILIA TEKNOLOJIA ZA JUU ZA KIDIGITALI NCHINI VIETNAM

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), akiambatana na ujumbe kutoka Tanzania ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TTCL,  Moremi Marwa  wamefanya ziara Viettel High Technology Industries jijini Hanoi, Vietnam.

 Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia fursa za ushirikiano katika teknolojia za 5G, Cybersecurity, Smart City, IoT na Artificial Intelligence (AI) ili kuharakisha ajenda ya mabadiliko ya kidijitali nchini.

TTCL kama mdau muhimu katika sekta ya mawasiliano liko tayari kuchukua fursa hizo ili kuboresha huduma zake kwa wateja na kuunga mkono dira ya Taifa ya kidijitali.

Viettel High Technology nao wamethibitisha utayari wao wa kushirikiana na Tanzania katika miundombinu ya mawasiliano, uhamishaji wa teknolojia na ujenzi wa uwezo.