info@ttcl.co.tz
+255 22 214 2000

TTCL QUEENS YAIBUKA MSHINDI WA TATU ATE

Timu ya Mpira wa Pete ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, (TTCL Queens) imeshiriki Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)

Katika Bonanza hilo team ya Mpira wa Pete (TTCL QUEENS) imecheza michezo miwili kati yake na OSHA pamoja na TPA.

Katika mchezo wake na OSHA, TTCL Queens ilipata magoli 10 kati ya 23 ya mpinzani wake huku ikipata magoli 10 kwa 13 iliyojishindia TPA na hivyo kuibuka Msindi wa Tatu wa Bonanza hilo.

Akizungumza katika michuano hiyo iliyofanyika kwenye Viwanja vya TTC Gwanbina Club, team captain Bi. Rachel alisema timu yake imecheza vizuri licha ya kukosa ushindi wa nafasi ya Kwanza na ya Pili

Alisema kukutana na kucheza na TPA pamoja na OSHA kumezidi kuwapa morali wachezaji wake kujituma zaidi ili watakapokuwa na mashindano mengine kwenye bonanza hilo waweze kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande wake Meneja wa TTCL Queens Bi. Getrude Kipengele alisema mchezo ulikuwa mzuri kwani timu zote zilionesha ushindani licha ya kuwa mchezo huo ulikuwa bonanza.

"Timu zote zimecheza vizuri na zimeonesha ushindani wa hali ya juu kwani kila mmoja alitaka team yake iibuke na ushindi" alisema Kipengele

Aidha aliongeza kuwa ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ijayo wanapaswa kuweka juhudi kubwa katika kufanya mazoezi binafsi na ya pamoja ili team iwe na muunganiko mzuri zaidi ya sasa.

Bonanza la Michezo limefunguliwa rasmi Septemba 9, 2023 na Kilele chake kitafanyika Oktoba 7 Mwaka huu ambapo Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi.