info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YASHIRIKI MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026 DODOMA

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2026 katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma.

Kupitia maonesho hayo, TTCL inatoa fursa kwa wananchi kujifunza kuhusu huduma mbalimbali za mawasiliano na suluhisho za kidijitali zinazotolewa na Shirika hilo, pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa TTCL kuhusu matumizi ya huduma hizo katika shughuli za kila siku, biashara na taasisi mbalimbali.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ni jukwaa muhimu linalowakutanisha taasisi mbalimbali za umma kwa lengo la kuonesha huduma wanazotoa, kuimarisha mahusiano na wananchi na kuongeza uelewa kuhusu mchango wa sekta ya umma katika maendeleo ya taifa.

Katika banda la TTCL, wananchi watapata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika, ikiwemo huduma za Faiba Mlangoni Kwako (FTTH), huduma za simu za mkononi, huduma za kifedha kupitia T-PESA, pamoja na suluhisho nyingine za mawasiliano na TEHAMA.

TTCL inawakaribisha wananchi wote kutembelea banda lake katika Viwanja vya Chinangali Park ili kujionea huduma na teknolojia mbalimbali zinazotolewa na Shirika na kupata taarifa zaidi kuhusu namna TTCL inavyoendelea kuchangia maendeleo ya Tanzania ya kidijitali.