TTCL YASHIRIKI TAMASHA LA KIJA 2026
Na Emerco Mashelle
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kwa kushirikiana na wadau, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na jamii, kuhamasisha matumizi ya teknolojia katika maisha ya kila siku.
Katika kuunga mkono juhudi hizo, TTCL imeshiriki Tamasha la Kinondoni Jogging Association (KIJA) 2026, lililofanyika Viwanja Vya Posta Kijitonyama likilenga kuwakutanisha wananchi katika shughuli za kijamii, afya na burudani.
Akizungumza wakati wa tamasha hilo, Msaidizi wa Meneja Mkoa Biashara kutoka Mkoa wa DSM N Bw. Atubonekisye Mwakagenda, amesema ushiriki wa TTCL katika Tamasha la KIJA ni sehemu ya jitihada za Shirika kuendelea kuwa karibu na jamii na wadau wake.
Amesema TTCL inaendelea kutumia fursa mbalimbali za kijamii kuwaelimisha wananchi kuhusu huduma za mawasiliano na suluhisho za kidijitali zinazotolewa na Shirika, huku akiwahimiza washiriki kutumia teknolojia kwa tija katika shughuli zao za kila siku.
Tamasha la KIJA 2026 limewakutanisha pamoja wapenzi wa jogging kutoka maeneo mbalimbali nchini, likiwa na lengo la kuhamasisha mtindo bora wa maisha, kujenga mshikamano miongoni mwa jamii na kutoa fursa kwa wadau mbalimbali kushirikiana na wananchi.
Ushiriki wa TTCL katika Tamasha la KIJA 2026 unaakisi dhamira ya Shirika ya kuendelea kushirikiana na jamii na wadau mbalimbali katika kuunga mkono shughuli zinazochangia afya, ustawi na maendeleo ya wananchi.