info@ttcl.co.tz
+255 22 210 0100

TTCL YATUNUKIWA CHETI CHA SHUKRANI KIZIMKAZI

Na Adeline Berchimance

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi cheti Meneja TTC Zanzibar Bi. Nasra Mugheiry , ishara ya kutambua mchango wa Shirika la Mawasiliano (TTCL) katika kudhamini, kushiriki na kuunga mkono Tamasha la Kizimkazi ambalo lilifikia kilele Agosti 14, 2026  Kizimkazi, Kusini Unguja, Zanzibar.

TTCL imekuwa sehemu muhimu ya kuwezesha tamasha hilo kufanyika kwa ufanisi kupitia miundombinu na huduma za mawasiliano, zilizosaidia kuwezesha mawasiliano na shughuli mbalimbali za kidijitali wakati wa tamasha.

Uwepo wa huduma za TTCL uliwawezesha washiriki, waandaaji, wafanyabiashara na wageni kuendelea kuwasiliana na kutumia fursa za kidijitali, hivyo kuchangia katika mafanikio ya tamasha hilo na kukuza matumizi ya teknolojia katika matukio makubwa.

Tamasha la Kizimkazi huwakutanisha wakazi wa Zanzibar, wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wageni kutoka Tanzania Bara na nje ya nchi, kwa lengo la kutangaza urithi wa kipekee wa utamaduni wa Kizanzibari, kukuza uchumi, kuhamasisha utalii na kuimarisha mshikamano.