TTCL YAZINDUA “SUPERSONIC EXPERIENCE; KASI BALAA” KWA HUDUMA YA FAIBA MLANGONI KWAKO
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi huduma mpya ya intaneti ya kasi kubwa inayojulikana kama “TTCL Faiba Supersonic Experience; Kasi Balaa”, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za kidijitali kwa Watanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL, Bw. Vedastus Mwita, amesema huduma hiyo inalenga kuongeza kasi, ubora na uhakika wa intaneti ili kuwasaidia wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kidijitali kwa ufanisi zaidi.
Huduma ya Faiba Mlangoni Kwako imeboreshwa kwa kuanzisha vifurushi vipya vyenye kasi kubwa kuanzia 60 Mbps hadi 250 Mbps, vinavyowawezesha wateja kufurahia matumizi ya intaneti kwa shughuli kama vile Smart Home, Smart Office, biashara mtandaoni, gaming, na streaming ya video za ubora wa juu (HD na 4K) bila kukatika.
Kupitia vifurushi hivyo, wateja pia watanufaika na dakika za simu za mezani pamoja na vifurushi vya intaneti kwa simu za mkononi, huku wakipatiwa SIM Card za TTCL bure kulingana na kifurushi watakachochagua.
Uzinduzi huu unaonesha dhamira ya TTCL kuendelea kuwa kinara katika ujenzi wa uchumi wa kidijitali nchini, kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye ubora, gharama nafuu na uhakika kwa Watanzania.