info@ttcl.co.tz
+255 22 214 2000

TUNA MATUMAINI MAKUBWA NA TTCL - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali inayo matumaini makubwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika kuleta mapinduzi kwenye sekta mbalimbali zinazotegemea mawasiliano ili kuendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya TEHAMA.

Waziri Mkuu Majaliwa ameonesha kufurahishwa na kazi inayofanywa na TTCL katika kutoa huduma za mawasiliano kwa Wananchi kwamba zinaridhisha na kwamba shirika hilo likiendelea na kasi ya utendaji wa kazi wa sasa ni wazi serikali itapata manufaa makubwa kupitia shirika hilo.

Waziri Mkuu aliyaema hayo alipotembelea banda la TTCL Mlimani City Dar es Salaam wakati wa Ufunguzi wa Siku ya Wahandisi Tanzania ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka ambapo akiwa bandani hapo alipata fursa ya kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga kuhusu kazi zinazotekelezwa na shirika hilo.

Mhandisi Ulanga amemwakikishia Waziri Mkuu kuwa TTCL imekuwa ikipiga hatua mbalimbali zikiwemo za kimkakati ili kuhakikisha mawasiliano yanawafikia Wananchi na hivyo kurahisisha utoaji wa huduma mbalimbali.

Amesema kwa sasa jumla ya 69 zimeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano huku ikitarajiwa ifikapo mwezi Januari 2024 idadi hiyo kuongezeka na kufikia 100 na ikitarajiwa ifikapo mwezi Juni kuzifikia Wilaya zote 139

Wahandisi nchini wamekutana kwa pamoja ili kuadhimisha Siku yao yenye lengo la kujadili sheria, kanuni, miongozo mbalimbali na maendeleo ya miradi inayohusu kazi za uhandisi ambapo pamoja na mambo mengine jumla ya wahandisi 200 wamekula kiapo cha kufanya kazi kwa weledi, nidhamu na kuzingatia maadili ya kazi ya uhandisi.

 

.