info@ttcl.co.tz
+255 22 214 2000

WI-FI YA BURE YAZINDULIWA BENJAMIN MKAPA STUDIUM

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya usimamizi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, limetekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan la kutaka Uwanja wa Benjamin Mkapa uwekewe huduma ya Mtandao wa Inteneti ikiwa ni sehemu ya ukarabati katika uwanja huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya Mtandao katika uwanja huo Novemba 5,2023, Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nnauye (Mb) alisema kutekelezwa kwa agizo hilo la Dkt. Samia linakwenda kuwasaidia mashabiki na wapenzi wa masuala ya michezo wote kufurahia uwepo wao kstika eneo hilo kwani watakuwa na uwezo wa kutuma na kupokea taarifa za matukio mbalimbali kiwanjani hapo kwa  kutumia intaneti yenye kasi zaidi.

“Leo tunaanza kuzindua huduma hii ya intaneti yenye kasi katika Uwanja huu wa Mkapa na kwa maagizo ya Rais Samia ya kwamba viwanja vyote vipate huduma ya mtandao ili wanaohudhuria viwanjani wafurahie Mtandao,” amesema Waziri Nape

Katika hatua nyingine Mhe.Nape amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) chini ya Mkurugenzi wake Mhandisi Peter Ulanga kwa kufanikisha uwekaji wa huduma hiyo katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Pigeni makofi ya kutosha kwa TTCL kwa kufanikisha hili la kuweka huduma hii ktaika uwanja huu na naamini kiwanja hiki ni ch kwanza na viwanja vingine vitafuata sasa mnawafanya mashabiki wafurahie kuja uwanjani kwa sababu wanafurahia huduma ya mtandao ambao nimefanyia majaribio na una kasi kwelikweli,”amesema Nape

Nape aliipongeza Azam Media Kwa kuendelea kurusha Matangazo ya mpira Kwa ubora Huku akiamini kuwa uwepo wa Mtandao WA uhakika kutoka TTCL itaendelea kunogesha Matangazo yao.

Uzinduzi huo uliudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo  pamoja na Katibu Mkuu  Gerson Msigwa.

Uzinduzi huo ilifanyika wakati wa mchezo kati ya Timu ya Simba na Yanga maarufu Derby ya Kariakoo ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Timu ta Yanga kushinda magori matano (5) dhidi ya goli 1 moja iliyojishindia Timu ya Simba.

UZINDUZI WA WI-FI YA BURE BENJAMIN MKAPA