Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga mazingira wezeshi kwa uchumi wa kidijitali Zanzibar kwa kuwezesha huduma ya intaneti katika mradi wa makazi wa Amani Residency, uliopo Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, kupitia huduma yake ya Faiba Mlangoni Kwako.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetajwa kuwa kinara katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano nchini, hatua inayothibitisha mafanikio ya uwekezaji wa muda mrefu katika miundombinu na mifumo ya huduma kwa wateja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemkabidhi cheti Meneja TTC Zanzibar Bi. Nasra Mugheiry , ishara ya kutambua mchango wa Shirika la Mawasiliano (TTCL) katika kudhamini, kushiriki na kuunga mkono Tamasha la Kizimkazi ambalo lilifikia kilele Agosti 14, 2026 Kizimkazi, Kusini Unguja, Zanzibar.
Tamasha la Kizimkazi 2026 limefikia kilele chake leo katika Viwanja vya Makunduchi, Zanzibar, likihudhuriwa na kufungwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasalimia Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) waliokuwa wakiliwakilisha Shirika katika banda la maonesho wakati wa Tamasha la Kizimkazi 2026.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa Makunduchi, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ametembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika Maonesho ya Tamasha la Kizimkazi 2026, ambapo amepata fursa ya kufahamu huduma na mchango wa TTCL katika kuimarisha mawasiliano na kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza wajibu wake wa kijamii na kitaifa kwa kuwapokea wanafunzi kutoka vyuo na kada mbalimbali nchini kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Field Attachment) kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuwakaribisha wananchi, wafanyabiashara, taasisi za umma na binafsi kutembelea banda lake lililopo Government Pavilion 2, Viwanja vya John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, ili kujifunza na kujionea kwa karibu huduma na suluhisho mbalimbali za kisasa za mawasiliano na Teknolojia.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), akiambatana na ujumbe kutoka Tanzania ikiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Moremi Marwa wamefanya ziara Viettel High Technology Industries jijini Hanoi, Vietnam.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) linaendelea kutoa huduma na elimu kwa wakulima na wananchi wanaotembelea Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika katika Uwanja wa John Malecela Nzuguni, jijini Dodoma.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetangaza ofa kabambe ya punguzo la bei kwenye vifaa vya intaneti kwa wananchi wanaotembelea banda lake katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nane Nane 2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mawasiliano nchini.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuonesha dhamira yake ya kuwekeza katika maendeleo ya rasilimali watu na kukuza kizazi kijacho cha wataalamu wa mawasiliano nchini kwa kuwapokea wanafunzi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), waliotembelea Makao Makuu ya Shirika jijini Dar es Salaam kwa mafunzo ya vitendo yaliyofanyika tarehe 30–31 Julai 2026.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza ujuzi wa teknolojia nchini kwa kutoa mafunzo ya kitaalamu kwa wanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu uendeshaji na usimamizi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Wanachama wa Kinondoni Jogging Association (KIJA) wametembelea Kituo cha Kidigitali Kijitonyama na kujionea kwa karibu namna teknolojia za kisasa na intaneti yenye kasi zinavyoweza kubadili maisha ya wananchi, kuimarisha biashara na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali.